Page 46 - Historiayatznamaadili
P. 46
Jamii za kale kabla ya ukoloni, zilitumia tiba za asili. Tiba hizo
zilitokana na mitishamba kama vile majani, mizizi, magamba
na magome ya miti. Pia, mafuta, ngozi na manyoya ya baadhi
ya wanyama vilitumika kama dawa. Dawa zilitumika kutibu kwa
FOR ONLINE READING ONLY
kunywa, kupaka, kufukiza, kuoga au kunusa. Kulikuwa na watu
rasmi waliokuwa na ujuzi na maarifa ya kutibu magonjwa kwa
kutumia dawa za asili. Mtu alipougua alipelekwa kwa mganga
kwa ajili ya matibabu na alipata huduma za tiba kama ilivyo
sasa. Ushauri wa tiba ulitolewa na wataalamu wa tiba wa jamii.
Mfano, kuna magonjwa ambayo mgonjwa alitakiwa kupumzika
na hata kula aina za vyakula kama tiba. Pia, tiba hizi zilihusisha
mazoezi mbalimbali katika mwili wakati wa matibabu.
Aidha, palikuwapo na huduma za afya ya uzazi ambazo zilitolewa
tangu pale kijana alipobalehe ili kumpa maarifa na stadi kwa ajili
ya uzazi bora. Vijana wa kike walifundishwa afya ya uzazi kuanzia
malezi ya mimba mpaka kujifungua mtoto. Pia, walifundishwa
chakula kinachofaa na jinsi ya kujilinda wakati wa ujauzito. Hii
ilifanyika ili kuwawezesha kupata uzazi bora na salama. Aidha,
palikuwa na watu rasmi waliohusika na shughuli za ukunga
katika jamii. Elimu ya afya ya uzazi ilisaidia uzazi salama na
kuepuka magonjwa yanayosababisha ukosefu wa uzazi.
Jamii za kale zilizingatia ulaji wa chakula bora kama sehemu ya
tiba. Matumizi ya dawa za asili na ulaji wa chakula bora, vilifanya
jamii za kale kuwa na afya imara. Afya ya jamii ilikuwa jambo la
kuzingatiwa sana katika jamii za kale.
Kazi ya kufanya namba 14
Andika mambo uliyojifunza kuhusu maendeleo ya
afya ya jamii kabla ya ukoloni.
39
06/11/2024 11:29:48
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 39 06/11/2024 11:29:48
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 39