Page 47 - Historiayatznamaadili
P. 47
Umuhimu wa maendeleo ya jamii kabla ya ukoloni
Maendeleo ya jamii kabla ya ukoloni, yalisaidia uendelezaji wa
shughuli za uchumi na jamii. Mfano, maendeleo ya jamii katika
elimu yalikuwa chanzo cha kuboresha maarifa na ujuzi wa jamii.
FOR ONLINE READING ONLY
Hivyo, kuongeza maarifa na ujuzi katika uzalishaji. Maendeleo
katika huduma za afya yaliboresha ustawi wa jamii, kwa jamii
kuwa na watu wenye afya njema katika ushiriki wa shughuli
za kijamii na kiuchumi. Vivyo hivyo, maendeleo katika makazi
yalisababisha jamii kuwa na mahali salama pa kuishi.
Zoezi la jumla
1. Andika NDIYO kwa sentensi iliyo kweli na HAPANA kwa
sentensi isiyo kweli.
(i) Maendeleo yaliyopo katika jamii zetu yaliletwa na
wakoloni _____________
(ii) Makazi ya jamii za kale yalitegemea shughuli za uchumi
na jiografia ya eneo linalohusika ________________
(iii) Mbinu ya vitendo ilitumika zaidi kufundishia na
kujifunzia kabla ya ukoloni____________
(iv) Jamii za kale tayari zilikuwa na dawa za kutibu
magonjwa mbalimbali katika jamii kabla ya ukoloni
________________
(v) Jamii zetu zilikuwa na maendeleo katika elimu, ingawa
mfumo wa kutoa elimu ulikuwa tofauti na huu tulionao
sasa____________
2. Taja mambo muhimu yaliyozingatiwa katika ujenzi wa
makazi kabla ya ukoloni.
3. Fafanua faida za elimu kabla ya ukoloni kwa maendeleo
ya jamii.
4. Eleza mbinu zilizotumika kutibu jamii kabla ya ukoloni.
40
06/11/2024 11:29:48
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 40
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 40 06/11/2024 11:29:48