Page 49 - Historiayatznamaadili
P. 49
Sura ya Sayansi na teknolojia za
Tatu asili kabla ya ukoloni
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Sayansi na teknolojia za asili zilikuwa na mchango mkubwa katika
maendeleo ya jamii kabla ya kuja kwa ukoloni. Katika sura hii, utajifunza
sayansi na teknolojia za asili kuhusu utengenezaji wa zana za mawe,
chuma na chumvi. Pia utajifunza kuhusu sayansi na teknolojia asilia za tiba
za asili, kilimo, uvuvi, ufinyanzi, ususi na uchongaji na maadili yake. Vilevile,
utajifunza michango ya sayansi na teknolojia hizo katika maendeleo ya jamii
na uchumi. Umahiri huu, utakuwezesha kuthamini sayansi na teknolojia
za asili kabla ya ukoloni na maadili yake. Hivyo, kutumia maarifa na ujuzi
huu katika kuendeleza shughuli za uchumi na jamii kwa sasa.
Fikiri
Sayansi na teknolojia ya asili katika jamii za
Kitanzania kabla ya ukoloni.
Dhana ya sayansi na teknolojia za asili
Sayansi na teknolojia za asili zinajumuisha matumizi ya
maarifa na ujuzi asilia wa wenyeji katika kuyakabili mazingira
yanayowazunguka. Maarifa na ujuzi ambao ulitokana na
utamaduni, rasilimali asilia, watu na vitu. Sayansi na teknolojia
asilia zilihusisha uvumbuzi, ubunifu na kufanya majaribio katika
kutengeneza zana na vifaa mbalimbali kwa lengo la kuyakabili
mazingira, kutatua matatizo, kurahisisha na kuboresha utendaji
wa shughuli katika jamii. Msingi wa sayansi na teknolojia asilia
ulikuwa kutafuta suluhisho la changamoto katika kukidhi mahitaji
ya jamii. Aidha, sayansi na teknolojia asilia ziliendelea kukua
kulingana na uhitaji wa jamii, mazingira na nyakati zilizohusika.
42
06/11/2024 11:29:49
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 42
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 42 06/11/2024 11:29:49