Page 53 - Historiayatznamaadili
P. 53
Kazi ya kufanya namba 2
Chunguza zana katika kielelezo namba 2 na 3, kisha
andika tofauti ya zana za Zama za Mawe za Kale
na za Kati.
FOR ONLINE READING ONLY
Pia, binadamu alianza kutengeneza nguo kwa kutumia ngozi
za wanyama. Sayansi na teknolojia ya utengenezaji nguo kwa
kutumia ngozi za wanyama ilifanywa kwa kuloanisha ngozi za
wanyama na kuzipondaponda ili ziwe laini, kisha kutengeneza
nguo. Aidha, katika Zama za Mawe za Kati binadamu aligundua
moto.
Sayansi na teknolojia ya asili ya kutengeneza moto
Sayansi na teknolojia ya kutengeneza moto iligundulika katika
harakati za utengenezaji wa zana, ambapo binadamu aligundua
uwapo wa cheche za moto wakati akigongagonga na kusugua
mawe. Pia, binadamu aliona cheche za moto zilizotokana na
radi, wakati radi ilipopiga. Hii ilisababisha binadamu kufanya
majaribio zaidi ya utengenezaji wa moto. Binadamu alianza kwa
kupekecha vijiti viwili vikavu ili kupata moto. Kielelezo namba 4,
kinaonesha sayansi na teknolojia ya awali ya kutengeneza moto.
Kielelezo namba 4: Sayansi na teknolojia ya asili ya kutengeneza moto
46
06/11/2024 11:29:51
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 46
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 46 06/11/2024 11:29:51