Page 56 - Historiayatznamaadili
P. 56

binadamu.  Sayansi  na  teknolojia  asilia  ya  Zama  za  Mawe
              iliboreshwa katika kila nyakati. Hivyo, kuboresha uwezo wa
              mwanadamu wa kupambana na mazingira na maisha yake.
              Kwa mfano:
          FOR ONLINE READING ONLY
                  (a)  Ugunduzi wa zana katika Zama za Mawe za Kale,

                       uliimarisha shughuli za uwindaji kwa kuongeza mazao
                       ya uwindaji;

                  (b)  Zana za mawe kipindi cha Zama za Mawe za Kati zilikuwa
                       bora zaidi, nyepesi na zilitumika kwa ajili ya kufanyia
                       kazi mahususi. Zana hizo zilitumika katika uwindaji na

                       kutengenezea nguo zilizotokana na ngozi za wanyama.
                       Pia, ugunduzi wa moto katika Zama za Mawe za Kati
                       ulileta maendeleo katika matumizi ya chakula. Aidha,
                       binadamu alitumia moto kuzuia baridi, hivyo, alianza
                       kuishi katika mapango; na


                  (c)  Zana za Zama za Mawe za Mwisho, zilileta maendeleo
                       zaidi katika shughuli za uvuvi na uwindaji. Zana hizo
                       zilimwezesha binadamu kuwinda wanyama zaidi na
                       kuvua samaki kwa urahisi ikilinganishwa na hapo awali.
                       Pia, zilitumika katika kilimo.


              Baadhi ya viashirio vya kuanza kwa shughuli za kilimo na ufugaji
              mwishoni mwa Zama za Mawe za Mwisho ni:
                      (i)  Kuanza kwa shughuli za kilimo za kuotesha au

                            kupanda mazao ya chakula na shughuli za ufugaji
                            wa wanyama wadogo. Hivyo, binadamu kupata
                            chakula cha kutosha;

                      (ii)  Binadamu kuanza kuishi katika makazi ya kudumu
                            kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji; na

                      (iii)  Kuibuka kwa uhitaji wa uongozi katika jamii. Pia,
                            huu ulikuwa mwanzo wa mgawanyo wa kazi baina
                            ya jinsi (kike na kiume) na marika (watoto, vijana
                            na wazee).


                                                   49




                                                                                          06/11/2024   11:29:52
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   49
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   49                                     06/11/2024   11:29:52
   51   52   53   54   55   56   57   58   59   60   61