Page 61 - Historiayatznamaadili
P. 61
Maadili katika sayansi na teknolojia asilia ya ufuaji wa chuma
Sayansi na teknolojia ya asili katika utengenezaji wa zana za
chuma ilihusisha maadili. Wahunzi walisali, walifanya matambiko,
waliimba na kunywa dawa za asili kabla ya kuanza ufuaji wa
FOR ONLINE READING ONLY
chuma ili kupata mazao bora ya chuma na kulinda afya zao.
Pia, uzalishaji wa chuma ulifanywa mbali kabisa na makazi ya
jamii hasa porini ili kuzuia watu kuvuta hewa chafu yenye moshi
uliotokana na fukuto wakati wa uyeyushaji wa chuma. Ufuaji wa
chuma ulifanyika katika tanuru ili kuzuia athari za moto mkali
kwa binadamu. Wanaume ndiyo waliohusika zaidi katika ufuaji
wa chuma. Hii ilitokana na imani za jamii katika upatikanaji wa
chuma na sababu za kiafya za afya ya uzazi kwa wanawake.
Sayansi na teknolojia ya chuma na maendeleo ya uchumi
na jamii
Sayansi na teknolojia asili ya chuma ilileta mapinduzi makubwa
katika sekta za uzalishaji mali na ulinzi katika jamii kabla ya
ukoloni nchini. Kwa mfano, majembe yaliboresha kilimo na
kuongeza uzalishaji katika kilimo. Binadamu alipanua mashamba
ya kilimo kwa kufyeka, kulima na kupanda mazao katika maeneo
makubwa zaidi. Upanuzi wa kilimo ulichangia kupatikana kwa
chakula na ziada. Upatikanaji wa chakula uliboresha afya ya
jamii, hali iliyoongeza afya ya uzazi na kusababisha ongezeko
la watu. Hivyo, kuimarika kwa shughuli za uchumi katika jamii.
Pia, afya bora ilisaidia kupunguza vifo vilivyotokana na lishe
duni. Ongezeko la watu lilisababisha uhitaji wa uongozi na watu
wenye mamlaka za uongozi katika jamii.
Utengenezaji wa zana za uvuvi kama vile ndoano ulisaidia
kuongeza mazao ya uvuvi. Utengenezaji wa vichwa vya mikuki
na mishale kwa kutumia chuma, kuliboresha shughuli za uwindaji
na zana za vita katika jamii. Aidha, sayansi na teknolojia ya
asili katika chuma ilisababisha kuibuka kwa mafundi sanifu
waliojulikana kama wahunzi. Wahunzi shughuli yao rasmi ilikuwa
54
06/11/2024 11:29:54
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 54 06/11/2024 11:29:54
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 54