Page 66 - Historiayatznamaadili
P. 66
Jamii zilizojihusisha zaidi na ufugaji ni Wamasai, Wadatoga,
Wajaluo, Wasukuma, Wairaqw na Wagorowa. Ufugaji ulifanyika
kwa kupeleka wanyama katika malisho mbali na makazi ya watu.
Mifugo iliwekwa katika maboma ambayo yalijengwa kwa kutumia
FOR ONLINE READING ONLY
nyasi, fito na matawi ya miba. Hii ilisaidia maboma haya kuwa
na hewa ya kutosha na mifugo kuwa na ulinzi dhidi ya magonjwa
na wanyama wakali.
Sayansi na teknolojia za asili zilitumika ili kufahamu majira ya
mwaka na viashirio vya ukame. Maarifa yalihusisha matumizi
ya mwezi na pepo. Hii ilisaidia wafugaji kupata malisho na maji
ya kutosha. Baadhi ya maeneo, wafugaji walijenga mabwawa
ili kukusanya maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Maeneo yasiyo na maji ya kutosha, walichimba visima vifupi ili
kupata maji.
Pia, walitumia maarifa asilia kujua tabia za wanyama na afya
zao. Mifugo ilitibiwa kwa kutumia mitishamba (dawa za asili).
Mbinu mbalimbali za kiasili zilitumika wakati wa kuchunga
mifugo. Mfano, mbwa waliofunzwa walitumika kuongoza
mifugo. Pia, miluzi ilitumika kuongoza mifugo na kuwasiliana na
wafugaji wengine. Palikuwako na aina tofauti za miluzi ambayo
iliwezesha wafugaji kutambua ishara mbalimbali, mfano vizuizi
dhidi ya wanyama wakali na kuwasiliana kwa kawaida. Mifugo
ilivikwa kengele kwa ajili ya ulinzi dhidi ya wanyama wakali.
Vilevile, sayansi na teknolojia za asili zilitumika katika uhifadhi
wa mazao ya mifugo. Mfano, maziwa yaliwekwa kwenye vibuyu
vya asili bila kuharibika. Miti maalumu ilitumika kusafishia vibuyu
vya kuhifadhia maziwa ili kuzuia yasiharibike. Pia, sayansi na
teknolojia asilia zilitumika kutengeneza samli kutoka katika
maziwa ya ng’ombe.
59
06/11/2024 11:29:55
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 59
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 59 06/11/2024 11:29:55