Page 69 - Historiayatznamaadili
P. 69
Kazi ya kufanya namba 9
Jadili namna ya kuendeleza sayansi na teknolojia
za uvuvi kwa jamii za sasa.
FOR ONLINE READING ONLY
Zoezi namba 3
1. Eleza tofauti ya sayansi na teknolojia za asili na za sasa
katika shughuli za uvuvi.
2. Bainisha faida za sayansi na teknolojia asilia katika uvuvi.
Sayansi na teknolojia asilia ya ufinyanzi
Sayansi na teknolojia ya ufinyanzi ilifanyika kwa kutumia udongo
wa mfinyanzi. Jamii zilikuwa na maarifa na ujuzi wa kutambua
udongo unaofaa na usiofaa kwa ajili ya shughuli za ufinyanzi.
Sayansi na teknolojia ya ufinyanzi ilifanyika kwa kutumia udongo
wenye asili ya mfinyanzi. Udongo huo ulichanganywa na maji,
kisha kuufinyanga kwa kuufinyafinya kwa lengo la kuunda
chombo chenye umbo fulani. Mfano wa vyombo vilivyofinyangwa
ni: mitungi, vyungu, bakuli na kadhalika. Kielelezo namba 14,
kinaonesha sayansi na teknolojia ya ufinyanzi.
Kielelezo namba 14: Sayansi na teknolojia ya ufinyanzi
62
06/11/2024 11:29:58
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 62
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 62 06/11/2024 11:29:58