Page 74 - Historiayatznamaadili
P. 74
Sayansi na teknolojia ya ufumaji ilifanywa kwa kufuma na kusuka
makuti, matete au majani ya mianzi ili kupata umbo fulani.
Kielelezo namba 22, kinaonesha makuti yaliyosukwa.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 22: Makuti yaliyosukwa
Kazi ya kufanya namba 11
Jadili namna ya kuendeleza sayansi na teknolojia
ya ususi katika jamii zetu kwa maendeleo ya sasa.
Sayansi na teknolojia asilia ya uchongaji
Sayansi na teknolojia ya asili ya uchongaji ilihusisha uchongaji
wa vifaa kama vile vinu, michi, bakuli, vijiko, sahani, miko, upawa,
meza, vigoda, chanuo, mipini, vitanda, viti na marimba za muziki.
Pia, ulihusisha uchongaji wa vyombo vya usafiri kwenye maji
mfano, majahazi, mitumbwi, ngalawa na makasia. Mfano wa
jamii zilizofanya shughuli za uchongaji wa vitu mbalimbali ni
Wamakonde, Wagogo, Wakimbu, Wanyamwezi, Wayao na
Waha. Jamii za Wayao na Wamakonde zilijihusisha zaidi na
uchongaji wa vitu vilivyotumika kwa mapambo.
Sayansi na teknolojia ya uchongaji ilitumia maarifa na ujuzi
67
06/11/2024 11:30:03
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 67
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 67 06/11/2024 11:30:03