Page 72 - Historiayatznamaadili
P. 72
kuhifadhia maji na nafaka. Aidha, vyombo hivi vilitumika katika
kubadilishana ili kupata bidhaa zilizokosekana katika jamii ya
wafinyanzi.
Kazi ya kufanya namba 10
FOR ONLINE READING ONLY
Jadili namna ya kuendeleza sayansi na teknolojia ya
ufinyanzi katika jamii zetu kwa maendeleo ya sasa.
Sayansi na teknolojia asilia ya ususi
Sayansi na teknolojia ya ususi ilifanywa kwa kutumia malighafi
kama vile ukindu, mianzi, matete, miwaa na majani ya minazi
na michikichi. Ususi ulifanywa kwa kusuka kitu. Mfano, makuti
ya minazi au chikichi yalisukwa kwa kutumia mikono au ukindu.
Ukindu ulitengenezwa kutokana na chale za minazi au michikichi.
Sayansi na teknolojia ya ususi ilifanyika kwa kupishanisha kindu,
mianzi, matete au majani ya minazi na michikichi kwa mpangilio
maalumu ili kupata umbo fulani. Kielelezo namba 19, kinaonesha
mfano wa kitanda kilichosukwa kwa makuti na kamba.
Kielelezo namba 19: Kitanda kilichosukwa kwa kamba za ukili na
makuti
Sayansi na teknolojia ya ususi kwa kutumia mianzi ilifanywa
kwa kutumia mianzi ambayo ilivunwa na kuchunwa kitaalamu,
65
06/11/2024 11:30:01
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 65
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 65 06/11/2024 11:30:01