Page 76 - Historiayatznamaadili
P. 76
Pia, jamii za Wapare zilitengeneza mashine asilia za kukamulia
juisi ya miwa kwa kutumia miti. Miti migumu miwili iliwekwa kwa
namna ya kupishana, na mti mrefu uliwekwa juu kwa ajili ya
kuizungusha mashine wakati muwa ukiwa katikati ya miti wiwili
FOR ONLINE READING ONLY
ili kukamua juisi. Kielelezo namba 24, kinaonesha mfano wa
mashine za asili za kukamulia juisi ya miwa.
Kielelezo namba 24: Mashine ya kukamulia juisi ya miwa
Kazi ya kufanya namba 12
Jadili namna ya kuendeleza sayansi na teknolojia ya
uchongaji kwa maendeleo ya jamii za sasa.
Sayansi na teknolojia asilia za utayarishaji chumvi
Jamii za kale zilitumia sayansi na teknolojia asilia kuzalisha
chumvi. Mfano, chumvi ilitengenezwa kwa kuchemsha maji
yenye asili ya chumvi. Baada ya maji kuchemka na kukaukia,
mabaki yake yalichujwa ili kupata chumvi.
69
06/11/2024 11:30:05
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 69
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 69 06/11/2024 11:30:05