Page 80 - Historiayatznamaadili
P. 80
Maadili katika sayansi na teknolojia asilia za tiba za asili
Sayansi na teknolojia ya utayarishaji wa dawa za asili ulifanywa
kwa kuzingatia maadili ambayo msingi wake ulikuwa ni wa siri
sana. Usiri ulifanyika ili kuficha utaalamu kwa baadhi ya watu
FOR ONLINE READING ONLY
ambao walijulikana kama waganga. Si kila mtu katika jamii alijua
namna ya kutengeneza dawa za asili. Uwezo wa kutengeneza
dawa ulikuwa kwa baadhi ya watu kwenye jamii. Wataalamu
wa tiba asili walirithisha ujuzi wao kwa watu waliowachagua.
Pia, utunzaji wa siri ulilenga kujali na kulinda utu wa wagonjwa.
Uadilifu, upendo na huruma vilikuwa miongoni mwa maadili
yaliyozingatiwa katika tiba asili. Sifa hizi zilikuwa za msingi kwa
kuwa tiba za asili zilihitaji wataalamu walio waadilifu. Tiba za asili
hazikuwa kwa ajili ya biashara katika jamii za kale, bali zilitolewa
kama huduma kwa wahitaji. Wagonjwa walitoa chochote kama
shukurani na haikuwa lazima. Pia, usafi ulizingatiwa katika
kutayarisha dawa hizi. Palikuwapo na kanuni maalumu za
utayarishaji wa kila dawa na matumizi yake. Mfano, palikuwepo
na dawa zilizotumika kwa kunywa, kuoga, kupaka, kunusa,
kujifukiza na za kuchanjiwa. Kimsingi, matumizi ya tiba za asili
yaliwezesha jamii kutibu magonjwa tofauti.
Zoezi namba 5
1. Taja faida za matumizi ya tiba za asili katika jamii.
2. Ainisha sayansi na teknolojia za tiba zilizotumika
kutengeneza dawa za asili.
3. Eleza maadili yaliyozingatiwa katika sayansi ya tiba za
asili katika jamii za kale.
Kazi ya kufanya namba 14
Fanya uchunguzi kuhusu mwendelezo wa sayansi
na teknolojia ya tiba za asili katika jamii yako kwa
sasa.
73
06/11/2024 11:30:08
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 73
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 73 06/11/2024 11:30:08