Page 81 - Historiayatznamaadili
P. 81

Sayansi na teknolojia asilia ya kutengeneza nguo
              Jamii za kale zilikuwa na nguo za asili zilizotengenezwa kwa
              kutumia ngozi za wanyama na magome ya miti. Magome ya miti
              yalibanduliwa kutoka katika miti maalumu iliyotumika kutengeneza
          FOR ONLINE READING ONLY
              nguo.  Sayansi na teknolojia ya kutengeneza nguo ilifanywa kwa
              kupondaponda magome ya miti
              kwa kutumia jiwe, vipande vya
              miti au kitu kigumu ili kuyalainisha
              na kupata nguo. Nguo hizi
              zilijulikana kama “mbungu” katika
              jamii za Wahaya. Pia, nguo za
              magome ya miti zilikuwapo katika

              jamii za Wamanyema, Waha, na
              Wahangaza. Kielelezo namba 27,
              kinaonesha magome ya miti
              yaliyotumika kutengenezea nguo.              Kielelezo namba 27: Magome
                                                           ya miti ya kutengenezea nguo


              Vilevile,  ngozi  za  wanyama  zilichunwa  na  kuanikwa,  kisha
              kuzilainisha kwa kupondaponda na kupaka mafuta ili kupata
              nguo.  Kielelezo namba 28, kinaonesha nguo za magome ya
              miti na ngozi za wanyama.























                    Nguo za magome ya miti                    Nguo za ngozi ya wanyama

                Kielelezo namba 28: Nguo za magome ya miti na ngozi za wanyama


                                                   74




                                                                                          06/11/2024   11:30:10
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   74
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   74                                     06/11/2024   11:30:10
   76   77   78   79   80   81   82   83   84   85   86