Page 86 - Historiayatznamaadili
P. 86
8. Eleza umuhimu wa kuendeleza maadili katika sayansi na
teknolojia za asili nchini Tanzania kwa sasa.
9. Je, ni kwa vipi sayansi na teknolojia za asili na maadili
yake zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo nchini
FOR ONLINE READING ONLY
kwa sasa?
Msamiati
Asili chimbuko, mwanzo au kiini cha kitu fulani
kutokea au kuanza
Anika kutandaza au kuweka kitu kwenye mwanga wa
jua au upepo kwa lengo la kukikausha
Banika kuweka kitu katika moto kikiwa juu ya wavu au
katika chuma
Chambo kitu, kama vile nyama, mdudu, samaki
kilichowekwa katika ndoano ili kutegea samaki
Kitali chumaghafi kitokanacho na uyeyushaji wa asili
wa chuma
Mbale madini yaliyowekwa katika tanuru kuzalisha
chuma
Kufinyafinya kuminyaminya kitu kwa kutumia vidole au
kiganja cha mkono
Kufinyanga kutengeneza kitu kwa kutumia udongo wa
mfinyanzi
Kukausha kuondoa unyevu au maji kutoka katika kitu kwa
kutumia jua, au njia nyingine ili kufanya kiwe
kikavu
Tiba kutibu au kuponya mgonjwa au mtu mwenye
matatizo ya kiafya kwa kutumia mbinu za
kitabibu
79
06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 79 06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 79