Page 87 - Historiayatznamaadili
P. 87
Sura ya Shughuli za uchumi
Nne kabla ya ukoloni
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Jamii za Kitanzania zilikuwa na shughuli mbalimbali za uchumi kabla ya kuja
kwa wakoloni. Katika sura hii, utajifunza kuhusu shughuli za uchumi kama
vile kilimo, uhunzi, ususi, ufinyanzi, uvuvi na maadili yake. Pia, utajifunza
mchango wa shughuli hizo za uchumi katika maendeleo ya jamii nchini
kabla ya ukoloni. Vilevile, utajifunza wajibu wa jamii katika kuendeleza
shughuli za uchumi. Umahiri utakaoupata utakusaidia kutambua shughuli
za uchumi na michango yake katika maendeleo ya jamii nchini, hivyo,
kuweza kuzithamini na kuziendeleza katika jamii zetu kwa sasa.
Fikiri
Shughuli za uchumi nchini na maadili yake kabla
ya ukoloni.
Dhana ya shughuli za uchumi
Kazi ya kufanya namba 1
Fanya uchunguzi kwa kuuliza au kutembelea maeneo
yenye shughuli za uchumi zilizofanyika katika jamii
inayokuzunguka kabla ya ukoloni.
Jamii zilijishughulisha na shughuli mbalimbali za uchumi kabla
ya ukoloni. Shughuli hizo ni kilimo, uvuvi, biashara, viwanda
na kadhalika. Shughuli hizo zilitofautiana kati ya jamii moja na
nyingine. Hii ilitokana na utofauti wa mazingira ya kijiografia
ambapo jamii iliishi, hali ya hewa, uwapo wa rasilimali asilia na
maarifa na ujuzi wa asili katika jamii husika.
80
06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 80
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 80 06/11/2024 11:30:10