Page 92 - Historiayatznamaadili
P. 92
samaki kutoka kwa jamii za wasusi. Vilevile, walibadilishana
samaki na jamii za wachongaji ili kupata mitumbwi na ngalawa
iliyotumika katika uvuvi. Hali kadhalika walibadilishana samaki
ili kupata chumvi kutoka kwa jamii zilizotengeneza chumvi. Hii
FOR ONLINE READING ONLY
ilisaidia kukua kwa shughuli za uchumi na biashara kabla ya
ukoloni. Kimsingi, palikuwa na maendeleo makubwa katika
shughuli za uvuvi kabla ya kuja kwa wakoloni.
Kazi ya kufanya namba 4
Jadili na kuandika mambo yaliyochangia kukua kwa
shughuli za uvuvi kabla ya ukoloni.
Wavuvi hoyee! Watu wote kwenye hadhara waliitikia hoyee!
Kisha kupiga makofi na vigelegele. Wageni walifurahi sana
kusikia kuhusu maendeleo hayo ya uvuvi.
Zoezi namba 2
1. Je, ni maendeleo yapi yaliyokuwapo katika shughuli za
uvuvi kabla ya ukoloni?
2. Eleza namna ya kuendeleza matumizi ya zana za uvuvi
na mbinu za uvuvi na uhifadhi wa samaki kwa sasa.
Shughuli za uchumi katika viwanda
Wageni kutoka jamii zilizojishughulisha na viwanda walieleza
kuhusu maendeleo ya shughuli zao kabla ya ukoloni. Shughuli
za uchumi katika viwanda zilihusu uhunzi, ufinyanzi, uchongaji,
ususi na utengenezaji chumvi.
Shughuli za uchumi katika uhunzi
Mzee Paukwa alielezea zaidi maendeleo ya shughuli za viwanda
zilizotokana na uhunzi. Mzee Paukwa alianza kwa kuelezea
kwamba:
85
06/11/2024 11:30:12
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 85
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 85 06/11/2024 11:30:12