Page 95 - Historiayatznamaadili
P. 95
Kazi ya kufanya namba 6
Jadili namna ya kuendeleza shughuli za ufinyanzi
nchini kwa sasa ili kukuza uchumi wa viwanda.
FOR ONLINE READING ONLY
Wafinyanzi hoyee! Alisema bibi Mkisi na kuhitimisha simulizi yake.
Hoyee! Wageni waliitikia huku wakipiga vigelegele na makofi.
Alifuata Mzee Pakawa wa kabila la Wandali ambaye alieleza
kuhusu shughuli za viwanda vya ususi.
Shughuli za uchumi za ususi
Mzee Pakawa alianza simulizi kwa kuelezea kuwa:
Jamii nyingi zilikuwa na maendeleo katika shughuli za viwanda
vya ususi. Viwanda vya ususi vilitengeneza vitanda vya kamba,
nyungo, nyavu za kuvulia samaki, vikapu, mikeka na kadhalika.
Vitu hivi vilitengenezwa kwa ajili ya shughuli za uchumi na
matumizi ya nyumbani. Mzee Pakawa alionesha mfano wa
vikapu vilivyotengenezwa katika viwanda vya ususi kama
vinavyoonekana katika Kielelezo namba 4.
Kielelezo namba 4: Vikapu
Shughuli za ususi zilifanyika kwa kutumia ukindu, miwaa, makuti
na mianzi. Pia, viwanda vya ususi vilitengeneza nyavu ambazo
zilitumika kama mitego ya kutegea wanyama na ya kuvulia
samaki. Mitego ilitengenezwa kwa kutumia nyuzi laini. Usukaji
wa bidhaa hizi ulitumia matete, miwaa, mianzi na makuti. Jamii
88
06/11/2024 11:30:13
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 88 06/11/2024 11:30:13
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 88