Page 90 - Historiayatznamaadili
P. 90
Shughuli za kilimo ziliambatana na uwepo wa maarifa na stadi za
kukuza na kuimarisha kilimo. Mfano, wakulima walifanya kilimo
cha matuta na ngoro ili kuzuia mmomonyoko wa udongo. Pia,
maeneo ya Engaruka, palikuwapo na kilimo cha umwagiliaji.
FOR ONLINE READING ONLY
Kilimo cha umwagiliaji kilifanyika kwa kuvuna maji ya mvua na
kuyatumia wakati wa ukame. Jamii za Wachaga pia zilifanya
kilimo cha umwagiliaji kwa kuweka mitaro ambayo ilitiririsha maji
kutoka maeneo yenye maji hadi kwenye mashamba kwa ajili ya
kilimo cha umwagiliaji. Kimsingi, jamii zilikuwa na maendeleo
makubwa katika shughuli za kilimo. Jamii zililima mazao kwa ajili
ya chakula na ziada. Ziada ilitumika kwa ajili ya kubadilishana
na jamii nyingine ili kupata bidhaa zingine. Jamii za wakulima
zilipata vitu kama vyungu, chumvi, zana za chuma na kadhalika.
Wakulima hoyee! Watu wote kwenye hadhara waliitikia hoyee!
Kisha kupiga makofi na vigelegele. Wageni walifurahi sana
kusikia kuhusu maendeleo katika kilimo.
Kazi ya kufanya namba 2
Jadili na kuandika mambo uliyojifunza kuhusu
shughuli za kilimo kabla ya ukoloni.
Zoezi namba 1
1. Eleza maendeleo yaliyokuwapo katika kilimo kabla ya
ukoloni.
2. Ainisha mambo ya kuendeleza katika shughuli za kilimo
kwa sasa.
Shughuli za uchumi katika uvuvi
Mgeni aliyefuata alikuwa mzee Kwere ambaye alizungumzia
shughuli za uchumi katika uvuvi. Mzee Kwere alieleza kuwa:
83
06/11/2024 11:30:12
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 83 06/11/2024 11:30:12
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 83