Page 89 - Historiayatznamaadili
P. 89
uwepo wa sayansi na teknolojia katika matumizi ya zana za
kilimo. Mwanzoni, kilimo kilifanyika kwa kiwango kidogo. Hali
hii ilitokana na uwepo wa zana duni za mawe na miti. Aidha,
kadiri zana za kilimo zilivyoboreshwa, ndivyo, shughuli za kilimo
FOR ONLINE READING ONLY
zilivyoboreshwa. Kielelezo namba 2, kinaonesha majembe ya
miti yaliyotumika awali kwa shughuli za kilimo.
Kielelezo namba 2: Majembe ya miti
Shughuli za kilimo zilishika kasi wakati wa ugunduzi wa chuma.
Ugunduzi wa chuma ulisababisha utengenezaji wa zana za
chuma kama vile majembe, mundu, mashoka na mapanga. Jamii
zililima eneo kubwa zaidi kwa kutumia zana hizi. Mfano, katika
maeneo ya Kagera kulikuwa na wakulima walioimarika kutokana
na matumizi ya zana za chuma katika kilimo. Wakulima hawa
walimiliki ardhi kubwa na kuikodisha kwa watu wengine kwa ajili
ya kilimo. Hali hii ilisababisha kukua kwa mfumo wa ukabaila
uliojulikana kama “Nyarubanja”. Wakulima wakubwa waliomiliki
ardhi walijulikana kama “Batwazi”. Pia palikuwapo na “Batwana”,
ambao hawakumiliki ardhi. Batwana waliishi kwa kulima maeneo
ya ardhi za Batwazi, kisha kuwapa Batwazi sehemu ya mazao
waliyovuna kama ushuru. Pia, jamii za Wachaga, Wapare,
Wasukuma na Wanyakyusa zilikuwa zimepiga hatua kubwa
katika shughuli za kilimo kabla ya kuja kwa wakoloni. Jamii
zililima mazao kama vile maharagwe, mtama, uwele, ulezi,
magimbi na ndizi.
82
06/11/2024 11:30:11
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 82
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 82 06/11/2024 11:30:11