Page 84 - Historiayatznamaadili
P. 84
kufuma nyavu na kusuka mitego ya samaki ambayo
iliendeleza uvuvi. Zana za chuma ziliwaibua mafundi wa
kuchonga ambao walichonga vyombo vya nyumbani kama
vile sahani, bakuli, vinu, miko na pawa. Pia, walichonga
vyombo vya uvuvi na usafiri kama mitumbwi na ngalawa;
FOR ONLINE READING ONLY
(c) Kuongezeka kwa uzalishaji wa ziada wa bidhaa
mbalimbali ndani na nje ya jamii. Ongezeko la bidhaa
lilisababisha watu kuanza kubadilishana bidhaa. Huu ukawa
ndio mwanzo wa watu kufanya biashara. Jamii za wakulima
zilibadilishana mifugo kwa nafaka kutoka kwa jamii za
wafugaji. Pia, wafugaji na wakulima walibadilisha bidhaa
zao ili kupata zana kutoka kwa mafundi sanifu; na
(d) Kuimarika kwa afya ya jamii. Wataalamu wa tiba asilia
waliwatibu wagonjwa waliokuwepo kwenye jamii. Udhibiti
wa magonjwa ulisababisha jamii kuwa na afya na kuweza
kushiriki katika shughuli mbalimbali za uchumi. Uwepo wa
tiba asilia na wataalamu wake kama wakunga, kuliwezesha
akina mama kujifungua salama. Uzazi salama ulisababisha
ongezeko la watu ambao ndiyo nguvu kazi katika jamii.
Hivyo, kuendeleza uchumi wa jamii.
Sayansi na teknolojia za asili zilichangia maendeleo endelevu ya
uchumi nchini kabla ya kuja kwa wakoloni. Sayansi na teknolojia
zilisimamia utunzaji wa mazingira na kuhimiza maadili ya jamii.
Hii ilisaidia kutunza mazingira kwa vizazi vijavyo, kukinga jamii
na magonjwa, kuongeza nguvu kazi na kuhifadhi utaalamu katika
jamii. Matumizi ya sayansi na teknolojia asilia yalisaidia kuleta
maendeleo ya uchumi na jamii ya muda mrefu.
Kazi ya kufanya namba 15
Jadili wajibu wa jamii katika kuendeleza sayansi na
teknolojia za asili kwa sasa.
77
06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 77 06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 77