Page 79 - Historiayatznamaadili
P. 79
Sayansi na teknolojia ya tiba za asili
Sayansi na teknolojia ya tiba ya asili zilitofautiana kutoka jamii
moja na nyingine. Sayansi na teknolojia ya tiba za asili zilitumia
mimea na wanyama ili kutayarisha dawa. Sehemu ya mimea
FOR ONLINE READING ONLY
iliyotumika ni mizizi, mbegu, majani, magome ya miti na maua.
Kielelezo namba 26, kinaonesha baadhi ya sehemu za mimea
na wanyama zilizotumika kutengeneza dawa za asili.
Kielelezo namba 26: Sehemu za mimea na wanyama zilizotumika
kutengenezea dawa za asili
Sehemu kubwa ya mimea hii ilipatikana katika mazingira ya jamii
husika. Sayansi na teknolojia ya utayarishaji dawa ilifanyika
kwa kuchukua mmea husika, kisha kuuchemsha, kuukausha,
kuuponda, kuutwanga, kuusaga, kuuchoma, au kuukwangua ili
kupata dawa. Pia, mmea ulichanganywa na maji, uji au supu na
kuchemshwa ili kupata dawa. Sayansi na teknolojia ya asili ya
utengenezaji dawa ilitumika ili kuifanya mitishamba hiyo iweze
kutibu kwa njia mbalimbali.
Dawa zilizotengenezwa kutokana na wanyama zilipatikana
kwa kuchemsha na kuchuja mafuta kutoka katika nyama
yenye mafuta, na mafuta hayo kutumika kama tiba. Pia, nyama
ilichemshwa ili kupata supu, ambayo ilitumika kama dawa.
Matumizi ya dawa yalitegemea aina ya dawa na ugonjwa husika.
Zipo dawa zilizotumika kama vimiminika baada ya kuchemshwa
na nyingine zilitumika katika hali ya unga. Dawa zilizochomwa
zilitumika katika hali ya majivu au mkaa.
72
06/11/2024 11:30:08
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 72
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 72 06/11/2024 11:30:08