Page 83 - Historiayatznamaadili
P. 83
salama, na ile ambayo haina harufu mbaya, ladha chungu
au yenye sumu. Wavuvi, hali kadhalika, walitumia nyenzo
salama kama nyavu, madema na ndoano ili kutunza mazao
ya samaki. Uhunzi ulifanyika mbali na makazi ya watu ili
kuzuia watu wasivute hewa chafu iliyotokana na moshi wa
FOR ONLINE READING ONLY
uyeyushaji chuma. Wanawake wajawazito hawakuruhusiwa
kuwa maeneo yenye tanuri la kuyeyushia chuma. Mwiko
huu uliwekwa ili kulinda afya ya wanawake kwa sababu
matanuru yalikuwa na joto kali ambalo ni hatari kwa afya
ya mama na mtoto awapo tumboni; na
(g) Matumizi ya sayansi na teknolojia yenye faida kwa jamii.
Hili lilizingatiwa kwa sababu teknolojia ilitokana na maarifa,
ujuzi na rasilimali asilia. Hivyo, jamii inayohusika ilikuwa
na haki ya kufaidika na teknolojia husika. Kwa mfano,
wataalamu wa tiba asilia hawakujitengenezea faida kwa
huduma walizotoa. Watu waliopatiwa tiba walitoa mifugo,
mazao au zana kama sehemu ya shukurani. Ubadilishanaji
wa mazao ya sayansi na teknolojia ulizingatia haki, usawa
na makubaliano.
Mchango wa sayansi na teknolojia asili katika uchumi
Sayansi na teknolojia za asili zilikuwa na mchango mkubwa kwa
maendeleo ya uchumi katika jamii za kale. Sayansi na teknolojia
za asili ziliendeleza uchumi kwa njia zifuatazo:
(a) Kuongeza ufanisi katika uzalishaji mali. Mfano, uvumbuzi
wa sayansi na teknolojia ya chuma, uliongeza ubora wa zana
katika kilimo, uwindaji na uvuvi. Wakulima walianza kulima
mazao katika eneo kubwa zaidi. Hii ilisaidia kupata mazao
mengi kwa ajili ya chakula na ziada ambazo zilitumika katika
biashara. Biashara ilizisaidia jamii kupata bidhaa ambazo
hawakuwanazo. Pia, kilimo kilisababisha ongezeko la idadi
ya watu kutokana na kuwapo kwa chakula cha kutosha na
lishe bora. Hii ilisababisha kuongezeka kwa nguvukazi.
Pia, zana hizo ziliongeza mazao katika uvuvi na uwindaji;
(b) Kuibua mafundi katika nyanja mbalimbali. Mafundi
hawa walikuwa tegemeo la wazalishaji mali wengine kwa
kuwatengenezea zana za kazi. Kwa mfano, wasusi waliweza
76
06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 76 06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 76