Page 88 - Historiayatznamaadili
P. 88
Shughuli za uchumi za jamii kabla ya ukoloni
Siku moja kiongozi wa jamii ya wakundi alifanya sherehe kubwa
ambayo alialika watu kutoka jamii zilizojishughulisha na shughuli
mbalimbali za uchumi. Hafla hii ilikuwa kwa ajili ya kuzitambua
FOR ONLINE READING ONLY
shughuli za kiuchumi zilizofanyika katika jamii zao na maadili
yake. Wageni waalikwa walikaa karibu na moto mkubwa
wakichoma nyama huku wakizungumzia kuhusu shughuli za
uchumi katika jamii zao kabla ya kuja kwa wakoloni. Kielelezo
namba 1, kinaonesha wageni toka jamii mbalimbali na bidhaa
zitokanazo na shughuli zao za uchumi.
Kielelezo namba 1: Wageni kutoka jamii mbalimbali
Shughuli za uchumi katika kilimo
Mgeni wa kwanza kuzungumza alikuwa mzee Mwaka ambaye
alizungumzia kuhusu shughuli za kilimo. Mzee Mwaka alianza
kwa kuelezea kwamba:
Shughuli ya uchumi katika jamii yetu ilikuwa kilimo. Shughuli
za uchumi za kilimo zilitofautiana katika jamii za wakulima
kulingana na mazingira, maarifa na ujuzi wa stadi za kilimo na
81
06/11/2024 11:30:11
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 81 06/11/2024 11:30:11
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 81