Page 93 - Historiayatznamaadili
P. 93
Uhunzi ilikuwa shughuli ya uchumi katika jamii kabla ya ukoloni.
Shughuli za uhunzi zilifanyika kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya
jamii na biashara. Baadhi ya jamii zilizojishughulisha na uhunzi
ni Wanyambo, Wahaya, Wazinza, Wafipa, Wapare, na Wayao.
Shughuli za uhunzi zilifanyika kwa wahunzi kufua chuma, kisha
FOR ONLINE READING ONLY
kutengeneza zana mbalimbali za chuma. Mfano, zana za chuma
zilizotengenezwa ni majembe, mashoka, mundu, mapanga,
mikuki na mishale.
Zana hizi zilichangia maendeleo katika shughuli za kilimo, uvuvi
na uwindaji. Pia, zana hizi zilileta mapinduzi katika silaha za
ulinzi. Zana za chuma kama vile mikuki na mishale zilitumika
kujihami dhidi ya maadui na wanyama wakali. Pia, zana hizi
zilitumika katika uwindaji kwa kuwawezesha wawindaji kupata
mawindo ya wanyama na kuwa na ziada. Viwanda vya uhunzi
vilikuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza shughuli
zingine za uchumi katika jamii kabla ya ukoloni.
Kazi ya kufanya namba 5
Jadili namna ya kuendeleza shughuli za uhunzi
nchini kwa sasa ili kukuza uchumi wa viwanda.
Wahunzi hoyee! Watu wote kwenye hadhara waliitikia hoyee,
kisha wakapiga makofi na vigelegele. Wageni walifurahi sana
kusikia kuhusu maendeleo ya shughuli za uhunzi.
Zoezi namba 3
1. Bainisha maendeleo katika shughuli za uhunzi kabla ya
ukoloni.
2. Fafanua mchango wa shughuli za uhunzi katika shughuli
zingine za uchumi kabla ya ukoloni.
Mgeni aliyefuata alikuwa Bibi Mkisi wa kabila la Wakisi
akiwakilisha jamii za wafinyanzi.
86
06/11/2024 11:30:12
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 86 06/11/2024 11:30:12
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 86