Page 94 - Historiayatznamaadili
P. 94

Shughuli za uchumi za ufinyanzi
              Bibi Mkisi alianza kuelezea kwa kusema:

              Jamii za wafinyanzi zilikuwa na viwanda vya kufinyanga vitu
              mbalimbali. Mfano wa vitu hivyo ni vyungu, bakuli, sahani na
          FOR ONLINE READING ONLY
              birika. Pia, jamii hizi zilitengeneza mitungi, tanuru na vibia.
              Vyombo hivi vilitumika kwa

              ajili ya matumizi mbalimbali
              kama vile kupikia, kuhifadhi
              maji, kuteka maji na kulia
              chakula. Jamii za wafinyanzi
              zilitengeneza vyombo imara
              kabla ya kuja kwa wakoloni.
              Mnaona vyombo hivi? Bibi
              Nyamasi alionesha baadhi
              ya vyombo vya mfinyanzi

              walivyotengeneza kama
              inavyoonekana katika                Kielelezo namba 3:  Vyombo vya
              kielelezo namba 3.                  ufinyanzi



              Vyombo hivi vilifinyangwa kwa kutumia udongo wa mfinyanzi.
              Jamii nyingi kwa sasa zinafanya shughuli za uchumi za ufinyanzi.
              Awali,  jamii  zilizokuwa  maarufu  kwa  shughuli  za  ufinyanzi
              ni Wakisi kutoka Kaskazini mwa ziwa Nyasa. Hali kadhalika

              Wapare kutoka Kilimanjaro na Wafipa kutoka Sumbawanga
              walikuwa maarufu kwa kazi za ufinyanzi. Vyungu vya Wakisi
              vilikuwa imara zaidi na havikuvunjika hovyo hovyo kwa sababu
              vilifinyangwa kwa udongo mzuri zaidi na vilikaushwa kivulini.


              Ufinyanzi ilikuwa shughuli kuu ya uchumi kwa jamii za wafinyanzi.
              Shughuli za ufinyanzi zilifanyika kwa ajili ya kukidhi mahitaji
              ya  jamii  na  biashara.  Biashara  zilifanyika  ili  kupata  bidhaa
              zilizokosekana katika jamii za wafinyanzi. Hii ilisaidia kuleta
              maendeleo katika jamii za wafinyanzi.






                                                   87




                                                                                          06/11/2024   11:30:13
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   87                                     06/11/2024   11:30:13
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   87
   89   90   91   92   93   94   95   96   97   98   99