Page 96 - Historiayatznamaadili
P. 96
za Wanyiha, Wandali, Wajita, Wahehe, Wahaya Wazaramo
na Wanyamwanga walikuwa maarufu kwa usukaji. Jamii hizi
zilibadilishana bidhaa za ususi na jamii zingine ili kupata bidhaa
ambazo hazikuwapo katika jamii zao.
FOR ONLINE READING ONLY
Mzee Pakawa alimaliza simulizi na wageni walishangilia kwa
vifijo.
Kazi ya kufanya namba 7
Fanya uchunguzi kwa kuuliza, kusoma matini au
kutembelea maeneo yenye shughuli za ususi na
kisha eleza namna ya kuziendeleza shughuli hizo
kwa matumizi ya sasa.
Shughuli za uchumi za uchongaji
Alifuata Mzee Kukawa kutoka jamii za Wamakonde. Yeye
aliwakilisha shughuli za uchumi katika viwanda vya wachongaji.
Mzee Kukawa alianza simulizi kwa kuelezea wageni kuwa:
Uchongaji ulikuwa ni shughuli kuu ya uchumi katika jamii
mbalimbali kabla ya ukoloni. Shughuli za uchongaji zilifanywa
kwa kuchonga vyombo vya chakula kama bakuli, sahani na
vijiko. Pia, jamii zilichonga vinu, michi, vigoda, marimba, chanuo,
pawa, vibakuli, miko na viti. Mzee Kukawa alionesha vyombo
vya kuchonga katika Kielelezo namba 5.
Kielelezo namba 5: Vyombo vya kuchonga
89
06/11/2024 11:30:13
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 89
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 89 06/11/2024 11:30:13