Page 101 - Historiayatznamaadili
P. 101
kuwa mahitaji yote ya shughuli za uchumi yalitokana na rasilimali
asilia katika mazingira yao. Jamii zilitambua kuwa rasilimali asili
ndizo zilizowapatia chakula, dawa (mizizi, majani na magome ya
miti) na malighafi kwa ajili ya shughuli za uchumi. Pia, rasilimali
asilia zilikuwa chanzo cha mvua. Hivyo, jamii ziliweka kanuni na
FOR ONLINE READING ONLY
taratibu za kimaadili katika ulinzi na matumizi ya rasilimali asilia
ili kuongeza ufanisi katika utendekaji wa shughuli za uchumi.
Aidha, maadili yaliendana na aina ya shughuli ya uchumi,
mazingira ya kijiografia na malighafi zilizotumika.
Maadili katika ulinzi wa rasilimali asilia
Miiko ilitumika kama sehemu ya maadili ili kulinda rasilimali
adimu zilizotumika kwa ajili ya uchumi. Miiko ilikataza watu
kukata aina fulani za miti, watu kulima katika vyanzo vya maji
kama vile, mito na maziwa. Pia, ilikataza kulima maeneo fulani
ya ardhi. Uhifadhi wa ardhi na misitu uliambatana na sheria za
mila zilizozuia kukata miti kiholela ili kupunguza uharibifu wa
misitu na kuhifadhi rasilimali asilia.
Jamii za wavuvi ziliweka taratibu za kipindi cha kuvua, maeneo
ya kuvua, na aina za samaki za kuvuliwa ili kuruhusu samaki
kuzaliana na kukua. Pia, ulinzi ulifanyika mazingira ya maji,
ili kuzuia uvuvi wa kupita kiasi na kuvua samaki wachanga.
Jamii za wakulima zilichoma vichaka katika eneo la shamba
jipya ili kuondoa uchafu na wadudu waharibifu. Pia, zilifanya
kilimo cha mseto ambapo mazao tofauti yalipandwa pamoja ili
kuongeza uzalishaji na kudumisha rutuba ya ardhi. Desturi hizi
ziliwasaidia kupunguza magonjwa ya mimea na hivyo kuongeza
mazao ya kilimo. Vilevile, mimea maalumu ilitumika kama dawa
katika kuzuia magonjwa na kuua wadudu katika mimea, ili kuzuia
athari za sumu kwa binadamu katika mazao. Aidha, wakulima
walichagua mazao bora na kuyahifadhi kama mbegu kwa ajili
ya msimu wa kilimo unaofuata. Maadili haya yalisaidia kulinda
afya ya jamii na kuhifadhi maeneo yenye rasilimali adimu kwa
shughuli za uchumi katika jamii, kwa faida ya jamii zao na vizazi
vijavyo.
94
06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 94 06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 94