Page 102 - Historiayatznamaadili
P. 102
Kimsingi, miiko hii ililenga kulinda uharibifu wa vyanzo vya
uchumi kama vile aina ya miti iliyotumika katika ujenzi, uchongaji
na dawa. Pia, ililenga kutunza vyanzo vya maji na rasilimali
zilizopo majini na kuhifadhi ardhi kwa matumizi ya baadaye.
FOR ONLINE READING ONLY
Zoezi namba 5
1. Bainisha maadili yaliyozingatiwa katika uvuvi ili kulinda
rasilimali za uvuvi kabla ya ukoloni.
2. Eleza umuhimu wa maadili katika uvuvi katika kuendeleza
uvuvi kabla ya ukoloni.
3. Eleza umuhimu wa maadili ya kilimo katika kuendeleza
kilimo kabla ya ukoloni.
Maadili katika kutunza afya ya jamii
Miiko iliwekwa ya kukataza kufanya shughuli za uhunzi maeneo
ya karibu na makazi ya watu. Hivyo, chuma kilifuliwa maeneo
ya misituni na katika matanuru yaliyosaidia kuongeza nguvu ya
joto na kupunguza moshi mkali utokanao na kazi ya kuyeyusha
chuma. Pia, wanawake wajawazito walizuiwa kuwa karibu na
maeneo yenye shughuli za uhunzi ili kuzuia athari za joto na moshi
mkali uliotoka katika tanuru kwa afya ya mama na mtoto. Vivyo
hivyo, shughuli zilizosababisha kuharibu mazalia ya samaki na
kuchafua vyanzo vya maji zilizuiliwa. Vilevile, palikuwapo na miti
maalumu iliyotumika katika shughuli za uchongaji. Hii ilisaidia
kuondoa matumizi ya miti ambayo ingeleta madhara kwa afya ya
binadamu. Wavuvi walitumia mbinu za uvuvi zilizolinda mazao ya
uvuvi. Mfano, walitumia mimea yenye kulevya samaki ili kuwavua
na siyo iliyoua samaki. Matumizi ya mbegu zilizohifadhiwa kwa
njia asilia katika kilimo yalisaidia kulinda afya ya jamii dhidi ya
magonjwa yatokanayo na sumu za mimea.
95
06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 95
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 95 06/11/2024 11:30:15