Page 104 - Historiayatznamaadili
P. 104
walifanya kazi pamoja kwa lengo la kusaidiana na kuongeza
ufanisi katika shughuli husika. Mfano, jamii zilisaidiana katika
shughuli kama vile kupanda, kuvuna, kuhifadhi mazao, uhunzi,
ufinyanzi, uvuvi na kadhalika. Hii ilisaidia kuongeza ufanisi katika
FOR ONLINE READING ONLY
kazi na kukuza uhusiano katika jamii husika. Aidha, jamii zilimiliki
shughuli za uchumi pamoja. Viongozi wa familia, ukoo au jamii
walikuwa wadhamini tu katika kusimamia shughuli za uchumi.
Watu wenye ujuzi, stadi na maarifa ya kufanya shughuli za
uchumi waliwafundisha vijana ili kurithisha maarifa na ujuzi
mahususi. Pia, shughuli za uchumi katika jamii zilifanyika kwa
siri kubwa ili kuhifadhi maarifa na ujuzi katika shughuli za uchumi
kwa jamii husika. Hii ilisaidia kuhifadhi maarifa na kuimarisha
utamaduni wa shughuli za uchumi kutoka kizazi kimoja hadi
kingine.
Zoezi namba 7
1. Ainisha maadili yaliyozingatiwa katika utendaji wa kazi
katika shughuli za uchumi.
2. Fafanua umuhimu wa maadili katika utendaji wa kazi
katika shughuli za uchumi.
Kazi ya kufanya namba 12
Jadili mambo uliyojifunza kuhusu maadili katika
shughuli za uchumi, kisha andaa mpango wa
kuyaendeleza katika jamii ya sasa.
Wajibu wa jamii katika kuendeleza shughuli za uchumi
Jamii ya sasa inao wajibu wa kupenda na kuthamini shughuli
za jamii zilizofanyika awali. Kila mwanajamii anao wajibu wa
kuzitambua shughuli za uchumi za kabla ya ukoloni na kufanya
kazi ili kuziendeleza katika jamii yake. Aidha, jamii inapaswa
97
06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 97 06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 97