Page 107 - Historiayatznamaadili
P. 107
Sura ya Ushirikiano na uhusiano
Tano wa kijamii na kiuchumi
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Ulipokuwa Darasa la Tatu ulijifunza kuhusu ushirikiano na uhusiano na
watu wengine katika jamii inayokuzunguka. Katika sura hii, utajifunza
kuhusu ushirikiano na uhusiano wa kijamii na kiuchumi kabla ya ukoloni.
Utajifunza misingi ya ushirikiano na uhusiano wa kijamii, ushirikiano na
uhusiano katika shughuli za kibiashara kati ya jamii na jamii na zile za
masafa marefu kabla ya ukoloni. Pia, utajifunza mchango wa ushirikiano na
uhusiano katika shughuli za kiuchumi katika maendeleo ya jamii kabla ya
ukoloni. Maarifa na ujuzi utakaoupata utakuwezesha kutambua umuhimu
wa ushirikiano na uhusiano katika maendeleo ya jamii ya sasa na baadaye.
Fikiri
Ushirikiano na uhusiano wa kijamii na kiuchumi
kabla ya ukoloni.
Dhana ya ushirikiano na uhusiano katika jamii
Kazi ya kufanya namba 1
Soma maana ya neno ushirikiano na uhusiano
kutoka vyanzo tofauti ikiwemo maktaba mtandao.
Uhusiano huelezea jinsi watu wanavyowasiliana na kujaliana
katika mambo mbalimbali. Watu wanaohusiana huwa na ukaribu
na lengo moja. Uhusiano unaweza kuwa kati ya mtu na mtu,
100
06/11/2024 11:30:16
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 100
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 100 06/11/2024 11:30:16