Page 109 - Historiayatznamaadili
P. 109
Zoezi namba 1
1. Eleza mambo uliyojifunza katika kujenga ushirikiano na
uhusiano mwema.
FOR ONLINE READING ONLY
2. Eleza jinsi misingi ya utu, heshima, upendo, ukweli,
uaminifu na amani inavyokuza na kutunza ushirikiano
na uhusiano.
Ushirikiano na uhusiano wa kijamii
Ushirikiano na uhusiano wa kijamii ulijengwa kwa kushirikiana
na kuhusiana katika shughuli za kijamii.
Kazi ya kufanya namba 4
Waulize wazazi au walezi kuhusu namna jamii za
kale zilivyojenga ushirikiano na uhusiano wa kijamii.
Ushirikiano na uhusiano kijamii katika misingi ya ujima
Ushirikiano na uhusiano katika jamii za awali kabisa ulikuzwa
katika misingi ya ujima. Ujima ni mfumo wa awali kabisa wa
kijamii, kiutawala na kiuchumi katika maendeleo ya binadamu.
Katika kipindi cha ujima watu wote walimiliki rasilimali kwa
pamoja na walifanya kazi pamoja. Kwa mfano, jamii zilishirikiana
katika shughuli kama vile kilimo, uvuvi, uwindaji na kadhalika.
Shughuli za kilimo na uvuvi katika kipindi cha ujima zilikuwa bado
ni za chini kutokana na ukosefu wa zana imara za uzalishaji
mali katika jamii. Zana zilizotumika katika kipindi hiki zilikuwa
zana za mawe. Mawe yalitumika kutengeneza zana kama vile
mikuki, mishale, mashoka, visu na kadhalika. Baadhi ya zana
hizi ziliwekwa mpini ili kurahisisha matumizi yake. Zana hizi za
mawe zilitumika katika kazi za uwindaji, kulima, kuchimba mizizi
na kusaga nafaka mbalimbali. Kielelezo namba 1, kinaonesha
binadamu aliyebeba zana za mawe zilizowekwa mpini.
102
06/11/2024 11:30:17
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 102
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 102 06/11/2024 11:30:17