Page 105 - Historiayatznamaadili
P. 105
kutambua misingi ya utendekaji wa kazi na maadili yake na
kuiendeleza katika jamii ya sasa.
Mapinduzi ya sayansi na teknolojia yatumike sambamba na
uendelezaji wa shughuli za uchumi kwa sasa ili kuleta maendeleo
FOR ONLINE READING ONLY
zaidi. Aidha, viongozi wa familia, ukoo au jamii wanapaswa
kusimamia shughuli za uchumi ili kuleta maendeleo kuanzia
ngazi ya chini kwa matumizi ya sasa na baadaye. Pia, usimamizi
huu utasaidia kuongeza ubunifu na ukuzaji wa viwanda na
kuongeza mianya ya ajira.
Kazi ya kufanya namba 13
Jadili na andaa mikakati ya kufuatilia uendelezaji wa
shughuli za uchumi katika jamii yako.
Zoezi la jumla
1. Taja maendeleo yaliyofikiwa na jamii katika shughuli za
kilimo kabla ya ukoloni.
2. Toa mifano ya viashirio vya maendeleo kwa jamii kabla
ya kuingia kwa ukoloni.
3. Taja faida ya shughuli za uchumi katika jamii kabla ya
ukoloni.
4. Bainisha maadili yaliyosisitizwa katika shughuli za uchumi
kabla ya ukoloni.
5. Je, kuna umuhimu gani wa kuendeleza maadili katika
shughuli za uchumi kabla ya ukoloni kwa sasa?
6. Eleza mambo ya kujifunza kutokana na shughuli za
uchumi kabla ya ukoloni.
98
06/11/2024 11:30:16
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 98
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 98 06/11/2024 11:30:16