Page 108 - Historiayatznamaadili
P. 108
familia na familia, jamii na jamii au Taifa na Taifa lingine.
Pia, ushirikiano huelezea namna watu wanavyofanya kazi au
shughuli fulani kwa pamoja. Kadiri watu wanavyoshirikiana,
ndivyo wanavyojenga uhusiano.
FOR ONLINE READING ONLY
Kazi ya kufanya namba 2
Andika mambo ya kuzingatia katika kujenga
ushirikiano na uhusiano mwema.
Ushirikiano na uhusiano hujengwa kwa misingi ya utu, upendo,
ukweli, uaminifu, amani na heshima. Pia, hujengwa kwa kuwa
na mawasiliano mazuri, kutembeleana mara kwa mara, kufanya
kazi kwa pamoja, kuepuka dhuluma na kujenga tabia ya
kuheshimu mipaka ya watu wengine. Watu wakiwa na uhusiano
mwema husaidiana, hupendana na huheshimiana. Ushirikiano
na uhusiano mwema haubagui jinsi, kabila, umri, dini wala
rangi. Ushirikiano na uhusiano mwema huleta mafanikio katika
maisha. Kwa hiyo, ni vizuri kujenga uhusiano mwema na watu
wanaotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku.
Kazi ya kufanya namba 3
Andika maana ya maneno utu, heshima, upendo,
ukweli, uaminifu na amani.
Tangu kale, jamii zilikuwa na ushirikiano na uhusiano kati yao
na jamii zingine. Ushirikiano na uhusiano huo ulijengwa katika
misingi ya utu, upendo, heshima, amani na ukweli. Jamii ziliepuka
dhuluma na ziliheshimu mipaka ya watu wengine. Hii ilisaidia
kujenga uaminifu katika jamii na kukuza uhusiano. Hapakuwa na
ubaguzi wala matabaka. Aidha, aina za ushirikiano na uhusiano
zilitofautiana na nyakati kulingana na maendeleo ya sayansi na
teknolojia.
101
06/11/2024 11:30:16
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 101 06/11/2024 11:30:16
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 101