Page 112 - Historiayatznamaadili
P. 112
Msingi wa mfumo huu wa uhusiano ulikuwa umiliki wa ardhi.
Mfumo huu ulienea maeneo yenye wakulima wakubwa, ambao
walimiliki ardhi na kuikodisha kwa watu wasio na ardhi katika
maeneo yao. Mfano wa mfumo huu ni Nyarubanja, katika
FOR ONLINE READING ONLY
jamii za Wahaya. Mfumo wa Nyarubanja ulihusisha tabaka la
Abatwazi ambao ni walimiliki wa ardhi na Abatwana ambao
walipewa ardhi na kufanya kazi kwenye maeneo ya Abatwazi.
Abatwana walilima na kuleta sehemu ya mazao kwa Abatwazi.
Pia, mfumo huu ulikuwapo maeneo ya jamii za Pwani ya Bahari
ya Hindi na ulijulikana kama Umwinyi Mkuu. Mwinyi Mkuu
alimiliki ardhi, mifugo na watwana. Watwana hawakumiliki
ardhi na hawakuruhusiwa kabisa kumiliki rasilimali katika jamii.
Hivyo, walikodi ardhi au mifugo kutoka kwa watawala ambao ni
“mamwinyi” na kurudisha sehemu ya mazao kwa Mwinyi kama
ushuru.
Mfumo wa ukabaila ndio ulioanzisha mizizi ya unyonyaji na
ubaguzi katika ushirikiano na uhusiano katika jamii za kale.
Misingi ya utu, upendo, usawa na amani ilianza kuondoka katika
ushirikiano na uhusiano wa jamii. Dhuluma na ubaguzi vilianza
kukua katika jamii. Jamii zingine zilizokuwa na mfumo huu ni
jamii ya Waha, Wapare, Wachaga, Wahangaza na Wanyambo.
Maeneo haya yote yalikuwa imara katika kilimo na ufugaji
kutokana na ugunduzi wa chuma.
Kazi ya kufanya namba 5
Jadili tofauti zilizokuwapo kati ya mfumo wa ujima
na ukabaila.
105
06/11/2024 11:30:17
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 105 06/11/2024 11:30:17
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 105