Page 115 - Historiayatznamaadili
P. 115
ya masafa marefu ilianza baada ya watu kuona haja ya kwenda
maeneo ya mbali zaidi ili kupata bidhaa ambazo jamii hazikuweza
kuzipata kutoka katika jamii za karibu. Mwanzoni biashara hii
ilihusisha jamii za wahunzi, wakulima, wasusi, wachongaji na
FOR ONLINE READING ONLY
wafinyanzi. Biashara hii baadaye ilikua zaidi na hata kuhusisha
jamii kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu. Biashara hii ilifanyika
maeneo ya Kaskazini, Kusini, Kusini Magharibi, Magharibi na
Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Tanzania.
Ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania; jamii zilizohusiana na
kushirikiana kibiashara ni Wapare, Wachaga, Wasambaa na
Wamasai. Wapare walikuwa maarufu katika biashara ya ukanda
wa Kaskazini. Hii ilitokana na umaarufu wa jamii ya Wapare katika
kutengeneza zana za chuma. Pia, jamii hii ilikuwa ya wafinyanzi
hodari wa vyungu. Hivyo, jamii hii ilibadilishana bidhaa zao na
Wachaga na Wasambaa. Kutoka kwa Wachaga walipata ndizi
na mazao mengine ya chakula. Wamasai walibadilishana na
Wapare mifugo ili wapate zana za chuma kama vile mikuki na
sime zilizotumika katika kulinda mifugo. Ushirikiano na uhusiano
wa biashara ya jamii hizi ulikwenda hadi kwa jamii za Wakamba
na Wataita walioishi Kenya.
Katika ukanda wa Kusini, uhusiano wa ushirikiano wa biashara
ulifanyika kati ya watu wa Pwani ya Msumbiji na ya Tanzania.
Biashara hii ilimilikiwa zaidi na jamii ya Wayao. Wayao
walibadilishana bidhaa kama majembe, tumbaku na vyungu na
jamii za Pwani ili kupata chumvi na mazao ya chakula. Biashara
hii ilivuka mipaka ya Tanzania hadi Malawi, Zambia na Angola.
Bidhaa muhimu baina ya nchi hizi na Wayao zilikuwa chumvi na
zana za chuma na shaba.
Upande wa Kusini Magharibi mwa Tanzania, jamii zilizohusiana
na kushirikiana kibiashara ni Wanyakyusa, Wakinga, Wakisi na
108
06/11/2024 11:30:18
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 108
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 108 06/11/2024 11:30:18