Page 118 - Historiayatznamaadili
P. 118
Baadaye, hasa kipindi cha karne ya 19, biashara hii ilihusisha
biashara ya utumwa na pembe za ndovu. Kielelezo namba
4, kinaonesha bidhaa za pembe za ndovu walizochukua
wafanyabiashara wakati huo.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 4: Pembe za ndovu
Pembe za ndovu zilitoka sehemu za mikoa yenye mbuga za
wanyama na kupelekwa Pwani ya Bahari ya Hindi. Vilevile,
wafanyabiashara hawa walichukua watumwa wachache kutoka
Pwani ya Bahari ya Hindi na kuwasafirisha kwenda nchi za
Mashariki ya Kati. Kutoka Mashariki ya Mbali na Kati,
wafanyabiashara hao walileta bidhaa kama vile nguo, shanga,
vyombo vya kauri na visu. Biashara hii ndiyo iliyosababisha kukua
kwa miji ya Bagamoyo, Kilwa Kivinje na Zanzibar.
Zoezi namba 4
1. Eleza mambo uliyojifunza kuhusu biashara ya masafa
marefu.
2. Eleza jinsi jamii za sasa zinavyoweza kuimarisha
biashara kwa kutumia stadi ulizojifunza.
111
06/11/2024 11:30:19
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 111
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 111 06/11/2024 11:30:19