Page 120 - Historiayatznamaadili
P. 120
Wapare walizalisha zana za chuma kwa wingi. Kadhalika jamii
za wachongaji, wafinyanzi na wasusi zilizalisha bidhaa zao
zaidi. Jamii hizo zilijishughulisha zaidi na shughuli za uchumi ili
kuendana na mahitaji katika biashara. Kimsingi, ushirikiano na
uhusiano wa kibiashara ulichangia kuendelea kwa shughuli za
FOR ONLINE READING ONLY
uchumi katika viwanda kama vile, ufinyanzi, uhunzi, uchongaji,
ususi na shughuli za kilimo kabla ya ukoloni.
Uhitaji wa bidhaa kwa ajili ya biashara ulisababisha kuibuka
kwa watu maalumu ambao kazi yao kubwa ilikuwa kufanya
biashara. Pia, biashara zilisababisha jamii kujifunza ujuzi na
stadi za jamii zingine. Jamii ziliiga stadi za jamii nyingine kwa
kuona na kutumia bidhaa za jamii zingine. Vilevile, uhusiano
wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wa masafa marefu na
jamii za Mashariki ya Kati na Pwani ya Afrika Mashariki ulichangia
kuenea na kukua kwa lugha ya Kiswahili. Lugha hii ilikuwa
kama hitaji la biashara ili watu kuweza kuwasiliana. Licha ya
kukuza lugha ya Kiswahili, biashara hii ndiyo iliyoeneza dini na
utamaduni wa Kiislamu kama vile uvaaji wa kanzu na baibui hasa
maeneo ya miji ya Pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya Ujiji
na Tabora. Hii ilitokana na wafanyabiashara kutoka Tabora na
Ujiji kushirikiana na wafanyabiashara hawa, haswa wakati wa
biashara ya utumwa.
Kazi ya kufanya namba 7
Fanya mdahalo kuhusu mada “jamii za Kitanzania
hazikuwa na maendeleo, ujio wa wakoloni ndio
ulioleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini”.
Jamii zilikuwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kabla ya kuja
kwa ukoloni nchini. Ukoloni haukuwa chanzo cha maendeleo
ya kiuchumi na ya kijamii nchini. Ukoloni ulileta mabadiliko ya
mfumo wa maisha nchini na sio mwanzo wa maendeleo nchini.
113
06/11/2024 11:30:19
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 113 06/11/2024 11:30:19
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 113