Page 119 - Historiayatznamaadili
P. 119
Kazi ya kufanya namba 6
Soma matini mbalimbali na maktaba mtandao kuhusu
mchango wa biashara ya masafa marefu katika
kukua kwa biashara ya wageni kutoka Mashariki ya
FOR ONLINE READING ONLY
Mbali na Kati kabla ya ukoloni.
Mchango wa uhusiano wa biashara katika uchumi na jamii
Ushirikiano na uhusiano wa biashara baina ya jamii na jamii na
ile ya masafa marefu ulileta maendeleo katika jamii zetu. Jamii
zilitumia bidhaa walizobadilishana kuimarisha jamii zao. Mfano,
jamii zilitumia silaha walizozipata kutoka kwa wahunzi kuimarisha
mfumo wa ulinzi katika jamii zao. Pia, biashara hizi zilisababisha
kukua kwa mamlaka za utawala wa jadi. Hii ni kutokana na
umiliki wa njia za biashara. Mfano wa mamlaka hizo ni tawala
za Wanyamwezi (Mtemi Isike na Mirambo) Wahehe (Mutwa
Mkwawa), Wayao (Chifu Machemba) na Wahaya (Omukama
Rumanyika). Viongozi wa jamii hizo walikusanya ushuru kutoka
kwa wafanyabiashara waliopita maeneo yao. Vilevile, tawala za
Umwinyi zilikua zaidi kutokana na uhusiano wa kibiashara haswa
na wageni kutoka Mashariki ya Kati.
Biashara hizi pia zilisababisha kukua kwa miji ya kifahari. Maeneo
ambapo biashara zilifanyika palijengwa majumba makubwa ya
mawe pamoja na misikiti na majumba ya kisultani. Maeneo hayo
ni Kilwa, Bagamoyo na Zanzibar. Miji ya Ujiji na Tabora ilikua
kutokana na biashara hii.
Biashara hizi, licha ya kuleta maendeleo ya kijamii, zilisababisha
kukua kwa shughuli za uchumi. Watu walizalisha bidhaa siyo
kwa lengo la kujikimu tu, bali kupata ziada kwa ajili ya biashara.
Hii ilisababisha kuwapo kwa watu ambao walizalisha bidhaa
kwa ajili ya biashara. Mfano, Uvinza ilianzisha kikundi ambacho
kazi yao kubwa ilikuwa kuzalisha chumvi. Wahaya, Wafipa na
112
06/11/2024 11:30:19
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 112
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 112 06/11/2024 11:30:19