Page 122 - Historiayatznamaadili
P. 122
Sura ya Mamlaka za jadi
Sita kabla ya ukoloni
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Mamlaka za jadi zilikuwa na mchango katika maendeleo ya jamii na
uchumi katika jamii husika. Katika sura hii, utajifunza kuhusu mamlaka
za jadi kama vile Uchifu, Ufalme, Utemi, Umwinyi, rika na ukoo kabla ya
ukoloni. Pia, utajifunza mbinu walizozitumia kutawala jamii za Kitanzania.
Vilevile, utajifunza michango ya mamlaka za jadi katika maendeleo ya
jamii zao. Umahiri utakaoupata utakujengea mbinu za uongozi na utawala
bora. Pia, utakuwezesha kuthamini mamlaka za jadi.
Fikiri
Mamlaka za jadi kabla ya ukoloni.
Viongozi wa jamii za jadi kabla ya ukoloni
Kazi ya kufanya namba 1
Waulize wazazi au walezi namna viongozi wa jamii
yako walivyopatikana na majukumu yao katika jamii
kabla ya ukoloni.
Jamii za Watanzania zilikuwa na viongozi shupavu na imara
kabla ya ukoloni. Karibu kila jamii ya Kitanzania ilikuwa na
kiongozi, mwenye mamlaka katika jamii yake. Uongozi huo
ulitofautiana kulingana na jiografia ya eneo husika, mahitaji ya
jamii na shughuli za uchumi. Viongozi hawa walijulikana kama
Machifu au Wafalme. Aidha, nyadhifa za machifu na wafalme
zilitofautiana kwa majina tofauti kutoka eneo moja hadi jingine.
115
06/11/2024 11:30:19
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 115
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 115 06/11/2024 11:30:19