Page 126 - Historiayatznamaadili
P. 126
Biashara ziliongeza ushujaa wa kivita kwa himaya ya Mtemi
Mirambo, kutokana na silaha kama vile bunduki ambazo walizipata
kutoka kwa wafanyabiashara kutoka Mashariki ya Kati. Mtemi
Mirambo alibadilishana pembe za ndovu na watumwa ili kupata
silaha. Pembe za ndovu zilipatikana kutokana na uwindaji wa
FOR ONLINE READING ONLY
tembo katika maeneo ya misitu. Watumwa walikuwa mateka wa
vita alivyopigana na jamii zingine wakati wa upanuzi wa himaya
yake. Mtemi Mirambo licha ya kufaidika na bidhaa za biashara,
pia alitoza ushuru kutoka kwa wafanyabiashara waliopita katika
himaya yake. Mtemi Mirambo alimiliki njia ya kati ya biashara ya
masafa marefu iliyoshirikisha wafanyabiashara kutoka Kongo,
Burundi, Rwanda na Buganda. (Rejea Kielelezo namba 3, katika
sura ya Tano). Ushuru uliopatikana kutoka kwa wafanyabiashara
ulichangia kukua na kuimarika kwa mamlaka ya Mtemi Mirambo.
Vilevile, jeshi la Mirambo lililojulikana kama “warugaruga”,
lilisaidia zaidi kuimarisha utawala wa Mtemi Mirambo. Jeshi hili
lilikuwa na nguvu kubwa kutokana na kuwa na silaha imara na
mbinu za kivita. Mtemi Mirambo alikuwa na nguvu kubwa za
kivita na aliweza kupinga wakoloni kuingia katika himaya yake.
Hii ilitokana na uwezo mkubwa wa kivita na utawala aliokuwa
nao. Hii ilisababisha wakoloni kumpa jina la “Napoleon wa
Afrika”, kutokana na uimara wake katika jeshi na vita.
Kazi ya kufanya namba 4
Jadili mambo uliyojifunza kuhusu utawala wa Mtemi
Mirambo na namna ya kuyaendeleza katika utawala
wa sasa.
Mtemi Isike
Mtemi Isike (1858-1893) alikuwa kiongozi wa jamii za
Wanyamwezi katika himaya ya Unyanyembe. Kiongozi huyu
alikuwa na utawala imara na nguvu kubwa ya kijeshi.
119
06/11/2024 11:30:20
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 119 06/11/2024 11:30:20
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 119