Page 130 - Historiayatznamaadili
P. 130
Kazi ya kufanya namba 6
Soma matini kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo
maktaba mtandao kuhusu mfumo wa uongozi ulipo
sasa nchini, kisha eleza mambo yanayofanana
FOR ONLINE READING ONLY
na kutofautiana na mfumo wa uongozi wa Mutwa
Mkwawa.
Vilevile, utawala huu ulikua kutokana na shughuli za biashara za
jamii na jamii na zile za masafa marefu. Kama ilivyokuwa kwa
watawala wengine, Mutwa Mkwawa alikusanya ushuru kutoka
kwa wafanyabiashara waliopita katika himaya yake kuelekea
Pwani ya Bahari ya Hindi kufanya biashara. Ushuru aliokusanya
ulisaidia kuimarisha utawala wake. Aidha, silaha zilizopatikana
ziliimarisha na kupanua zaidi himaya yake.
Mamlaka ya Mutwa Mkwawa ilikuwa ni imara nchini hata kabla ya
kuja kwa wakoloni. Kama ilivyokuwa desturi ya jamii hii kupinga
uvamizi na kulinda himaya yao, Mutwa Mkwawa hakuwa tayari
kuruhusu uvamizi wa wageni katika eneo lake. Mtemi Mkwawa
aliongoza watu wa jamii yake chini ya jeshi lake imara kupinga
uvamizi wa Wajerumani katika himaya yake. Mfano, mwaka
1891 Mtemi Mkwawa aliongoza jeshi lake na kuangamiza zaidi
ya askari 300 wa jeshi la Wajerumani, pamoja na kamanda wa
jeshi hilo Emil Von Zelewiski. Uimara wa jeshi la Mtemi Mkwawa
ulizuia utawala wa Wajerumani kuingia kwenye himaya yake
kwa zaidi ya miaka minne.
Kazi ya kufanya namba 7
Jadili mambo uliyojifunza kuhusu utawala wa Mutwa
Mkwawa na namna ya kuyaendeleza katika utawala
wa sasa.
123
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 123 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 123