Page 132 - Historiayatznamaadili
P. 132
hazikupatikana katika maeneo yao. Kimsingi, utengenezaji wa
zana za chuma ulisababisha kustawi kwa biashara katika eneo
la maziwa makuu. Hii ilitokana na utawala wa Kifalme kujihusisha
katika biashara na jamii za jirani. Biashara hii kwa kiwango kikubwa
FOR ONLINE READING ONLY
ilisababisha dola hizi za Kifalme kuwa imara na zenye nguvu.
Ujio wa Waarabu katika biashara za masafa marefu, ulikuta
tawala za Kifalme zinamiliki biashara. Wafalme ndio waliokuwa
kiunganishi cha wafanyabiashara toka bara na Pwani ya Bahari
ya Hindi. (Rejea kielelezo namba 3, sura ya 5). Umiliki wa
biashara ulisaidia kukua kwa himaya za Wafalme. Hii ilitokana
na ushuru walioutoza kwa kila mfanyabiashara aliyepita maeneo
ya falme hizi. Wafanyabiashara walilazimika kulipa kodi, mazao
na vito vya thamani kwa Mfalme. Ushuru huo ulisaidia kujenga
zaidi himaya za Kifalme kwa mali na nguvu za kijeshi. Jamii za
Kifalme zilikuwa katika hatua kubwa ya maendeleo kabla ya
ukoloni.
Omukama (mfalme) Rumanyika
Omukama Rumanyika ni miongoni mwa viongozi wa kifalme
waliotawala jamii za Buhaya. Neno Omukama lina maana ya
Mfalme au mkubwa wa wote. Jamii ziliwatambua viongozi wake
kwa jina hili kwa kuwa walikuwa na nguvu ya mali katika jamii.
Wafalme walimiliki biashara, ardhi, chuma na mifugo. Jamii
zilitegemea vitu hivi kutoka kwa Wafalme. Watu hawakuwa na
umiliki wa ardhi na mifugo. Hivyo, walipaswa kufanya kazi kwa
mfalme ili kupata mali na mazao. Wafalme ndio waliowapa
watu maeneo ya kulima na pindi walipovuna, walipaswa kuleta
sehemu ya mavuno hayo kwa Mfalme kama malipo.
Umiliki mkubwa wa ardhi katika jamii za Kifalme ndiyo uliokuza
mfumo wa ushirikiano na uhusiano katika jamii uliojulikana kama
Nyarubanja. Mfumo huu ulikuwa na tabaka la Abatwazi ambao
walimiliki ardhi, na Abatwana ambao walimilikiwa na Abatwazi
125
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 125 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 125