Page 127 - Historiayatznamaadili
P. 127
Utawala wa himaya hii ulikua kutokana na biashara za masafa
marefu zilizofanyika kupitia himaya yake hadi Pwani ya Bahari ya
Hindi. Biashara hizi zilimsaidia Mtemi Isike kupata silaha imara
na hivyo, kujenga jeshi la
FOR ONLINE READING ONLY
Unyanyembe, lenye nguvu,
silaha imara na mbinu za
kivita. Mtemi Isike alikuwa
na ngome imara ya kivita
katika ikulu ya Itetemya.
Hii ilimwezesha kiongozi
huyu kujilinda na kupiga
utawala wa Wajerumani
walipovamia himaya yake
ya Unyanyembe. Kielelezo
namba 2, kinaonesha picha
ya Mtemi Isike. Kielelezo namba 2: Mtemi Isike
Kiongozi huyu alipigana na Wajerumani kwa muda mrefu, zaidi
ya miaka minne. Jeshi la Wajerumani halikuweza kumshinda.
Aidha, Wajerumani walifanikiwa kuzingira himaya yake na
kumvamia baada ya kusalitiwa na watu wake wa karibu. Mtemi
Isike alijiua yeye na familia yake katika ngome yake. Mtemi Isike
alikuwa ni kiongozi shupavu na imara, usaliti ndio ulisababisha
kushindwa kwake.
Mtemi (chifu) Litti Kidanka
Mtemi Litti Kidanka ni mwanamke shujaa aliyeongoza kabila la
Wanyaturu. Mtemi Litti alijulikana Unyaturuni kote kwa sababu ya
nguvu na msimamo wake. Shujaa huyu hakuwa tayari kuruhusu
wageni kuingia katika himaya yake na kuleta utamaduni wa
kigeni. Mtemi Litti aliongoza mgomo wa Wanyaturu sehemu ya
Kaskazini, dhidi ya Wajerumani, kutokana na ushujaa wake.
Kiongozi huyu alipambana na Wajerumani kwa muda mrefu
120
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 120 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 120