Page 124 - Historiayatznamaadili
P. 124
kitemi zilijishughulisha na kilimo cha msimu na ufugaji. Shughuli
za ufugaji na kilimo zilihitaji kuongeza maeneo zaidi ili kukidhi
mahitaji ya jamii zao. Hivyo, viongozi wa jamii za “Watemi”
walifanya uvamizi katika jamii zingine ili kujenga utawala wao.
FOR ONLINE READING ONLY
Mambo yaliyosababisha kukua kwa tawala za Watemi
Shughuli za kilimo na ufugaji zilikuwa na mchango mkubwa
katika kukua kwa utawala wa Watemi. Aidha, ugunduzi wa
chuma, uliosababisha upatikanaji wa zana kama vile, mashoka,
visu, mapanga, majembe, mundu, mishale na mikuki ulisaidia
zaidi tawala hizi kuimarika. Zana hizo ziliimarisha zaidi shughuli
za kilimo na ufugaji. Hivyo, kuongezeka kwa uzalishaji katika
jamii na kuwa na ziada. Pia, ugunduzi wa chuma ulizisaidia
mamlaka za jadi kupata zana kama vile mikuki, mishale na
pinde zilizotumika kama silaha za vita katika uvamizi wa jamii
zilizowazunguka na kuweza kumiliki maeneo makubwa zaidi.
Vilevile, ukuaji wa jamii za Kitemi ulichangiwa na ushiriki katika
biashara za jamii na zile za masafa marefu. Jamii za Kitemi
zilishiriki biashara hizi na kupata bidhaa mbalimbali zilizosaidia
kukua kwa mamlaka zao. Aidha, ujio wa wafanyabiashara
kutoka Mashariki ya Mbali na Kati katika Pwani ya Bahari ya
Hindi kulichangia zaidi kukua kwa mamlaka za Watemi nchini.
Wafanyabiashara hawa walikuta wafanyabiashara wa jamii za
Kitemi wakifanya biashara toka ndani ya nchi hadi Pwani ya
Bahari ya Hindi. Hivyo, ukawa mwanzo wa wafanyabiashara
wa kigeni kuanza kufanya biashara na jamii za Watemi.
Biashara hizi ziliwezesha jamii za Kitemi kupata silaha kama
vile bunduki na vitu vingine mfano nguo, shanga na visu kutoka
kwa wafanyabiashara hao. Wafanyabiashara hawa wa kigeni,
hasa Waarabu, walipata malighafi kama vile pembe za ndovu,
vipusa, ngozi za wanyama na watumwa kutoka kwa wenyeji.
Bidhaa hizi zilichangia kukua kwa mamlaka za Kitemi. Kwa
mfano, silaha kama vile visu na bunduki zilitumika kuimarisha
majeshi ya watawala wa Watemi.
117
06/11/2024 11:30:20
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 117 06/11/2024 11:30:20
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 117