Page 129 - Historiayatznamaadili
P. 129
kwa jina la “Mukwavinyika” lenye maana ya “Mtemi wa ardhi”.
Kielelezo namba 4, kinaonesha picha ya Mutwa Mkwawa.
Kama ilivyokuwa viongozi wengine
wa utawala wa Watemi, Mutwa
FOR ONLINE READING ONLY
Mkwawa alipigana vita na makabila
mengi yaliyomzunguka ili kuongeza
umiliki zaidi wa ardhi katika eneo
alilotawala.
Kiongozi huyu alikuwa na nguvu
kubwa ya kijeshi hata kupewa jina la
“shujaa wa vita”. Kiutawala alikuwa
kiongozi mwenye nguvu za kivita
Kielelezo namba 4: Mutwa
na mwenye kuheshimiwa na jamii Mkwawa, mtemi wa Wahehe
yake.
Utawala wa Mutwa Mkwawa ulikua kutokana na uvamizi wa kivita
katika maeneo yaliyowazunguka. Mfano, Mutwa Mkwawa aliweza
kutawala eneo kubwa sana kuanzia kusini mwa Mpwapwa hadi
Malangali karibu na Mbalali. Pia, Mutwa Mkwawa alikuwa na
mfumo wa uongozi imara uliosaidia katika uongozi na utawala
wake. Viongozi katika utawala huu walishirikiana ili kuongeza
ulinzi, kutawala na kudhibiti uvamizi wa wageni. Kielelezo namba
5, kinaonesha mfumo wa utawala wa Mutwa Mkwawa.
Mtemi Kiongozi mkuu
Wanamhala Mkutano wa wazee wa ukoo
Wakusanya kodi
Minula
Msimamizi masuala ya imani
Nganwe
Mpelelezi
Mtwale
Kielelezo namba 5: Mfumo wa uongozi wa mutwa Mkwawa
122
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 122 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 122