Page 133 - Historiayatznamaadili
P. 133
na kulazimika kuleta sehemu ya mazao kwa Abatwazi kama
malipo. Shughuli za kilimo ziliimarisha tawala za Kifalme.
Jamii za Buhaya chini ya Omukama Rumanyika, pia, zilikuwa na
umaarufu katika kufua chuma. Hii ilisaidia kukua kwa utawala
FOR ONLINE READING ONLY
huu kutokana na jamii zingine kuhitaji zana za chuma kwa wingi.
Jamii za Buhaya na Karagwe zilibadilisha zana za chuma ili
kupata bidhaa zingine. Jamii hizi zilifanya biashara na jamii
kama vile Wanyamwezi, Wasukuma na Waha. Pia, zilifanya
biashara na jamii za mbali, Mfano, falme za Uganda kama vile,
Bunyoro na Ankole na maeneo ya Buganda ili kupata ng’ombe.
Aidha, ukuaji wa tawala za kifalme ulisababishwa na uwapo
wa mfumo imara wa uongozi. Kielelezo namba 6, kinaonesha
mfumo wa uongozi wa Kifalme.
Omukama Kiongozi mkuu (mfalme)
Katikiro Waziri mkuu
Mawaziri
Batongole
Baraza la washauri
Lukiko
Wakuu wa eneo (mkoa)
Bami B’enshonzi
Mwenyekiti wa kijiji
Bakungu
Kielelezo namba 6: Mfumo wa uongozi, tawala za kifalme (Buhaya)
Mfano wa mfumo huu wa utawala ulikuwapo katika jamii za
Wapare, ambapo kiongozi mkuu alikuwa Mfumwa (chifu)
akifuatiwa na baraza la wazee Mnjama, Wakuu wa vijiji Chila
au Mchili na chini walikuwapo walinzi na askari.
126
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 126 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 126