Page 137 - Historiayatznamaadili
P. 137
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 8: Mangi wakiwa katika boma la Wajerumani
Zoezi namba 1
1. Eleza mambo uliyojifunza kutokana na mfumo wa
uongozi wa Kifalme, Kitemi na Mangi.
2. Taja sababu zilizosababisha Wafalme, Mangi na Watemi
kuwa na nguvu kubwa katika jamii walizozitawala.
Umwinyi Pwani ya Afrika Mashariki
Utawala wa Umwinyi ulishamiri sehemu za Pwani hasa katika
maeneo ya Kilwa, Mafia na Bagamoyo. Pia, ulikuwepo maeneo
ya Unguja na Pemba kwa upande wa Zanzibar. Watawala
hawa walijulikana kwa majina tofauti kufuatana na sehemu
walizozitawala. Watawala walioishi sehemu za kati, Magharibi
na Kusini ya Unguja walijulikana kama Mwinyi Mkuu ikiwa na
maana ya mkuu wa eneo. Watumbatu waliwaita Sheha na
Pemba waliitwa Madiwani au Wajumbe.
130
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 130
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 130 06/11/2024 11:30:22