Page 141 - Historiayatznamaadili
P. 141
kiuchumi na kijamii. Pia, zilikuwa na mamlaka katika maeneo
yao na watu waliowatawala.
Viongozi walisaidia katika kukusanya ushuru kutoka kwa
wafanyabiashara waliopita na kufanya biashara katika maeneo
FOR ONLINE READING ONLY
yao na kuutumia kuimarisha himaya zao. Aidha, mamlaka za
jadi zilifanya biashara zenye faida kwa watu wao. Hii ilisaidia
jamii hizi kuwa na nguvu za uchumi. Pia, mamlaka za jadi
zilihamasisha shughuli za uzalishaji mali. Hii ilisaidia jamii zao
kuzalisha bidhaa kwa ajili ya matumizi na kuwa na ziada ambazo
ziliwezesha biashara. Ziada ilitumika katika biashara ili kupata
bidhaa zilizokosekana kwao. Hii ilisababisha maendeleo ya jamii
zao.
Vilevile, mamlaka za jadi zilikuwa na mchango mkubwa sana
katika kukuza maadili ya jamii zao. Viongozi hawa walisimamia
maadili katika jamii yao kama vile, heshima, kufanya kazi kwa bidii,
ushirikiano, upendo, usawa na umoja. Pia, walikuwa wasuluhishi
wa migogoro ndani ya jamii zao. Watu wote waliokwenda kinyume
na maadili ya jamii walichukuliwa hatua kwa kupewa adhabu.
Aidha, mamlaka za jadi zilisimamia ustawi wa watu na jamii.
Mfano, matumizi bora ya rasilimali, kama vile maji, ardhi na
misitu. Pia, walikuwa ni viongozi wa dini. Hivyo, walisimamia
miungu ya jamii zao. Mamlaka za jadi zilisimamia na kuhakikisha
ulinzi na usalama wa jamii zao na masuala ya mila na utamaduni
katika eneo lao.
Kimsingi, mfumo wa utawala wa mamlaka za kijadi ulikuwa na
mchango mkubwa sana katika maendeleo ya kijamii. Mamlaka
za jadi zilikuwa na utamaduni mzuri wa kutawala kwa kugawana
madaraka. Mgawanyo wa madaraka ulileta mafanikio katika
ulinzi na kuwapatia wanajamii mahitaji yao ya msingi. Pia,
mifumo hii ya utawala ilitumika kutatua migogoro katika jamii
na kusimamia ulinzi na usalama wa jamii.
Kazi ya kufanya namba 12
Andika mambo uliyojifunza kuhusu mamlaka za jadi na
jinsi ya kuyaendeleza ili kuboresha uongozi wa sasa.
134
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 134 06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 134