Page 139 - Historiayatznamaadili
P. 139
rika mbili muhimu: wazee na vijana. Wazee ndio waliokuwa na
madaraka ya mwisho kabisa katika jamii ya Wamasai. Kiongozi
wa kundi la wazee alijulikana kama Olaiboni, kundi hili lilitoa
ushauri kwa makundi mengine na hakuna kitu kilichokuwa
FOR ONLINE READING ONLY
kinaweza kufanyika katika jamii bila idhini ya rika hili la wazee.
Pia, kundi hili la wazee lilikuwa na wajibu wa kusuluhisha
migogoro iliyokuwa inatokea katika jamii yao. Kundi la vijana
lilijulikana kama morani na lilihusisha vijana wenye umri kati ya
miaka 18 na 35. Kundi hili ndilo lililokuwa nguvukazi ya jamii.
Kundi hili lilihusika na ufugaji kama vile, kutafuta maji na malisho
ya mifugo yao. Pia, walikuwa ndio walinzi wa mali na usalama
wa jamii nzima. Morani walitegemea sana ushauri wa wazee
chini ya Olaiboni katika kutekeleza majukumu yao. Aidha, wazee
chini ya Olaiboni ndio waliokuza na kutunza maadili ya jamii hizi.
Utawala wa kiukoo
Baadhi ya jamii kabla ya ukoloni zilikuwa zinajitawala katika
ngazi ya ukoo. Jamii hizi ni zile ambazo hazikuwa zimefika hatua
ya kuunganisha koo mbalimbali na kupata himaya za Uchifu na
Ufalme. Jamii hizi ziliongozwa na mkuu wa ukoo. Wakuu wa
ukoo walijulikana kwa majina tofauti tofauti kulingana na koo zao.
Jamii zilizokuwa na utawala wa kiukoo ni zile zilizoishi maeneo
ya Kusini Mashariki mwa Tanzania. Mfano wa jamii hizo ni:
Wamatumbi, Wamwera, Wangido, Wamakonde, Wandendeule,
Wakisi, Wapangwa na Wamakua.
Kimsingi, jamii za kabla ya ukoloni zilikuwa na mamlaka za
uongozi imara zilizotawala jamii kisiasa, kiuchumi na kimaadili.
Mamlaka hizi zilikuwa na nguvu imara za uongozi na ulinzi.
Hivyo, kuweza kuongoza na kulinda himaya zao. Mamlaka za
jadi zilitofautiana kati ya kabila na kabila. Kielelezo namba 9,
kinaonesha mtawanyiko wa baadhi ya makabila nchini.
132
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 132
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 132 06/11/2024 11:30:22