Page 135 - Historiayatznamaadili
P. 135
Sababu za ukuaji wa tawala za Mangi
Uwepo wa ardhi yenye rutuba na mvua za kutosha ilikuwa sababu
mojawapo ya kukua kwa tawala za Mangi kabla ya kuja kwa
ukoloni. Jamii hizi zipo karibu na Mlima Kilimanjaro, maeneo
FOR ONLINE READING ONLY
yenye mvua za kutosha na udongo wenye rutuba. Jamii hizi
zilijishughulisha na kilimo. Hivyo, ardhi ilikuwa kichocheo kikubwa
cha maendeleo na uchumi. Pia, ugunduzi wa chuma ulisaidia
kukua kwa tawala za Mangi. Jamii hizi zilitumia zana za chuma
katika kilimo kama vile majembe, mapanga, mundu na mashoka
kutoka jamii za Ugweno. Matumizi ya zana za chuma katika kilimo
yalisaidia maendeleo ya kilimo. Jamii za Wachaga zililima na
kupata mazao ya chakula na ziada. Ziada zilitumika kwa ajili
ya biashara. Jamii hizi zilifanya biashara na jamii za Wapare,
Wakamba na Wasambaa kwa kubadilishana mazao ya chakula
ili kupata zana za chuma na bidhaa zingine.
Jamii za Kimangi, kama zilivyokuwa jamii za Kitemi, zilijenga
himaya zao kutokana na kupigana na koo zingine ili kuongeza
himaya. Hii ilisababisha vita kati ya jamii hizi mara kwa mara.
Mfano, Mangi Sina wa Kibosho alipigana na Mangi Marealle
wa Marangu mara kwa mara. Mangi Sina alipigana na Mangi
wa Machame. Vita hivyo vilikuwa na lengo la kuongeza himaya
zao. Kiongozi aliyeshindwa alinyang’anywa ardhi na mifugo na
himaya yake ilichukuliwa na Mangi mwingine. Watawala wenye
nguvu ndio walioshika maeneo makubwa ya utawala. Ujio wa
wakoloni ulikuta tawala za Mangi zikiwa na maendeleo katika
kilimo, biashara na ufugaji. Pia, zilikuwa na nguvu kubwa ya
kijeshi. Mfano, Mangi Meli alikuwa na jeshi imara katika himaya
yake ya Old Moshi. Hivyo, kupinga utawala wa Wajerumani
katika eneo lake.
Mangi Meli
Mangi Meli alipinga uvamizi wa Wajerumani katika himaya yake
kutokana na uimara wa jeshi lake. Kielelezo namba 7, kina picha
ya Mangi Meli.
128
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 128 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 128